Header Ads

test

SABA SABA 2012: KUTAKUWEPO NA BANDA LA KUUZA BIDHAA ZA MAREHEMU KANUMBA

Miezi takribani mitatu tangu atangulie mbele za haki, familia ya marehemu mwigizaji Steven Kanumba imeamua kufanya jambo lingine la kuweza kumuenzi marehemu kupitia sanaa.
Kwa mujibu wa mdogo wa marehemu Kanumba, Seth, amesema kwenye maonyesho ya biashara ya saba saba mwaka huu wameamua kuchukua banda ambalo litauza na kuonyesha vitu mbalimbali vya The Late Steven Kanumba.

 
"Tumeamua kufanya hivi kwani tunadhani itakuwa nzuri zaidi kwa watu tofauti kumuenzi kipenzi chao kwa njia sahihi kabisa. Pia kwenye maonyesho ya sabasaba kunakuwa na watu kutoka sehemu tofauti ulimwenguni hivyo kupitia banda hilo tutapata nafasi ya kuuza na kuonyesha kazi mbalimbali za Kanumba kwa watu tofauti."


Seth ambae ni Mdogo wake waliekua wakiishi pamoja Sinza Dar es salaam amesema ni banda la Kanumba litakalokua na Nguo zenye alama alizokua anazitumia Kanumba ikiwa ni pamoja na jina na ujumbe, kutakua na picha zilizo kwenye frame za Kanumba zinazomuonyesha toka akiwa utotoni, pia vikombe, kanga, bazee na vitu vingine vingi vyenye alama na picha za Kanumba.
Seth amesema Mama mzazi wa Kanumba pamoja na watu aliokua akifanya nao kazi Kanumba watakuwepo kutoa maelezo mbalimbali kuhusu Kanumba na kazi zake.