JINSI WAZIRI MKUU ALICHOMJIBU FREEMAN MBOWE BUNGENI KUHUSU DR ULIMBOKA.
Waziri mkuu Mizengo Pinda
amesema serikali imeagiza kuzingatiwa sheria ya vifo vyenye utata kwa
kufanyika uchunguzi wa kina juu ya vifo hivyo ambapo pia amekanusha
stori kwamba Tanzania imechafuka kwenye anga za kimataifa kutokana na
matukio mbalimbali yaliyotokea.
Hii ni stori kutoka 104.4
Dodoma bungeni wakati akijibu swali la kiongozi wa kambi ya upinzani
Freeman Mbowe kwenye maswali ya papo kwa papo ambapo ameamlfy kwamba
kuwepo kwa hisia kuwa serikali inahusika katika mauaji ya raia sio
sahihi na hata ishu ya Kiongozi wa Madaktari Dr Ulimboka Steven
kujeruhiwa vibaya na watu wasiofahamika sio vizuri ikatumiwa kama mfano.
Freeman Mbowe alimuuliza waziri
mkuu kwamba “Mheshimiwa Waziri mkuu katika nchi yetu kwa muda mrefu
sasa yamekuwepo mauaji mengi na baadhi ya vifo hivi vimekua na utata
mkubwa na baadhi ya vifo hivi vimekua vikihisiwa kuhusisha vyombo vya
dola kama vile jeshi la Polisi, lakini ni kweli kwamba hisia za dola
kuhusika katika mateso na mauaji ya raia zimeendelea kuwepo na jinsi
ninavyouliza swali hili sifa ya taifa letu iko mashakani katika anga za
kimataifa kutokana na mateso ambayo yanaonekana yalikua na kusudio la
mauaji ambayo alifanyiwa mwenyekiti wa madaktari Dr Steven Ulimboka”
Alichojibu Waziri mkuu ni
hiki….. “Sio kweli kwamba jina la nchi yetu limechafuka, kuchafuka sana
kwa lipi? ukisema hivyo ni lazima vilevile uwepo ushahidi wa dhati
unaoonyesha kwamba ni kweli serikali inahusika, sasa umetumia mfano wa
Ulimboka… sio mfano mzuri, we huna ushahidi kama ni serikali imefanya
hivyo na hakuna mpaka sasa anaeweza kusema ana ushahidi huo, ndio maana
tulisema mara ya mwisho kwamba ni vizuri jambo hili likafanyiwa
uchunguzi wa kina ili tujue kilichotokea hasa ni kitu gani”
Kwa kumalizia kumjibu Freeman
Mbowe, Waziri mkuu amesema “hainiingii kichwani hata kidogo kwa mtu
ambae tumekua tunafanya nae kazi muda wote alafu sisi hao hao tuchukue
hatua tena ya kutaka kwenda kumuadhibu kwa namna iliyotokea, haiingii
kichwani”
Kwenye sentensi nyingine ni
kwamba Waziri Mkuu amesema serikali imefanya jitihada kubwa katika
kuwekeza kwenye sekta ya Afya hasa kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili
ambako hivi karibuni taasisi ya moyo itazinduliwa, ameamplfy pia kwamba
hatua nyingine ni kuipandisha hadhi hospitali ya Jeshi Lugalo ili kuwa
hospitali ya rufaa.
chanzo cha story Millardayo Blog
Post a Comment