No Church in the Wild’ ya Kanye West na Jay-Z yatoka ikiwa na ujumbe mzito
Hatimaye video ya wimbo mpya wa Kanye West na Jay-Z, “No Church in the Wild” imetoka.
Video hiyo inawaacha mashabiki na ujumbe mzito hata kama nguli hao wawili hawaonekani kwenye video.
Kwa mujibu wa MTV uamuzi huo wa Kanye na Jay-Z kutooenekana kabisa
kwenye video hiyo iliyoongozwa na Romain Gavras umekuwa na faida kwakuwa
kama wangeonekana, ujumbe waliotaka kuuwakilisha usingefika kwa
walengwa kama walivyotarajia.Muda kidogo
kabla ya mdundo haujaanza kusikika, wanaonekana vijana (wengi wanafunzi
wa kiafrika wanaosoma jamhuri ya Czech) wakiwa wamevalia vinyago
wakitembea kwa ‘slow motion’ kuelekea kwenye ukuta wa polisi
waliojiandaa kwa kuvaa nguo maalum kupambana na waandamanaji.
Kichapo kinaanza kikisindikizwa na mlipuko mkubwa wa bomu kwenye mtaa
wa mjini mkuu wa Czech Prague. Gavras anaonesha nguvu ya mapambano
inayotokea kila kona ya dunia iwe maandamano ya Misri, Libya, Tunisia
(mwaka jana) Los Angeles 1992 hata London mwaka 2011.
Waandamaji wasio na woga wanaonekana wakirusha mawe na kupigana na
polisi wenye silaha kwa kutumia mikono mitupu. Katika scene moja, polisi
anaonekana akimkimbiza kwa farasi mwanamapinduzi mmoja anayeanguka na
kuambuliwa kichapo cha ‘rungu.’
Vijana wanaonekana wakipigwa na kuburuzwa chini huku kiitikio
kilichokaa kisoul cha Frank Ocean kwenye ngoma hiyo kikisika taratabu
juu ya mdundo uliopikwa na Yeezy mwenyewe, “Will he make it out alive?”
Mwisho kabisa mwa video hiyo yenye dakika tano, wapigania uhuru wanaonekana kupata ushindi kwa kiasi fulani.
Hata hivyo, japo wameshinda vita, hakuna mwisho unayomaliza yote, ikimaanisha kuwa mapambano bado yanaendelea.
Post a Comment