Header Ads

test

  BADO ANA 17, KWA MUJIBU WA ALIOONA CHETI CHAKE CHA KUZALIWA

Atakuwa anazo sababu za kuamua kudanganya umri na mengineyo...... labda kama akipewa nafasi ya kuzungumza tunaweza kujua zaidi ana matatizo gani huyu binti jamani.
 
Tusiwe wepesi wa kuhukumu panapohitajika msaada basi asaidiwe
Kiwanda cha sanaa ya burudani,(Muziki, cinema) kina vishawishi vingi sana, usipo kuwa imara na hasa kwa wasichana wadogo wanaokuwa hawana msimamo katika maisha yao, au wanaokuwa wanatoka katika familia duni na wanahitaji kuzisaidia familia kwa njia moja au nyingine....
Watu wazima wanapatwa na vishawishi na wanashindwa kuvivuka, tunayaona kila siku.
Sembuse mtoto mdogo kama Lulu?
Huyu ni mmoja tu tunaemjua, lakini wapo wengi ambao ni wajeruhiwa na wanahitaji msaada katika swala kama hili.
 Ungana na Mhe. Halima Mdee (Mbunge Kawe, CHADEMA) kwenye twitter @halimamdee na kupata ufafanuzi na maelezo ya ziada ikiwa yatahitajika.

Mara zingine inaweza kuwa inachangiwa na wazazi pia
Ukiona mtoto wa mwenzio anapotea sio kupigilia msumari aendelee kuangamia bali kujaribu kumuokoa.