Header Ads

test

ALICHO ANDIKA LADY JAY DEE


Raha ya kuwa na chombo kama hiki uwe unajua jinsi ya kukitumia.
Kwasababu utakitunza na kukipenda na hutaruhusu mtu akuharibie.
Na mtu akibeba akadondosha hata kukikwangua kwa bahati mbaya unaweza ukalia siku nzima kwa kusikitikia hicho kitendo lol!

Katika maisha lazima uwe na ndoto za kufikia malengo fulani.
Hata kama ni magumu, au huna uhakika kama utaweza kuyatimiza malengo hayo.
Kujaribu na kujiamini ni muhimu na ndio njia ya kufikia malengo (kukamilisha ndoto), Ila kusema "siwezi" ni kushindwa kabla hujaanza.

Mwaka jana tu, nilikuwa naweza kugusa gusa ila sijui ninachokigusa ni nini.
Na wala hakikuwa kinaleta maana yoyote, wala hakijawahi kutengeneza hata melody ya wimbo wangu wowote ule.

Kwa kifupi nilikuwa nagusa kinanda na kinaleta sauti ambazo hazina maana yoyote, kwa maana nilikuwa sijui kupiga.

Sijafikia kiwango cha juu kwani ndio nahesabu kama nimeanza.
Lakini leo naweza kuthubutu kukaa chini na kujipongeza kidogo kwa kuweza kupiga japo Super Trouper ya Abba.
Mbali na hilo, Na kubwa zaidi naweza kusoma maandishi yalioandikwa kwa lugha ya kimuziki.
Ambayo zamani niliona kama urembo urembo flani tu hivi.
Tunachelewa kujua mengi kutokana na jamii tunayokulia kuchelewa kukubaliana na kazi tunazofanya. Ila kadri siku zinavyoenda sidhani kama mtawakataza watoto wenu wasifanye muziki kama wanapenda na wanaweza.

Ni lazima iwepo mifano miwili, mitatu kwanza ya ku prove mafanikio ndio wanaofuata wataaminiwa kufata njia hizo.
Naamini ipo siku nitapokea maua mengi tu ya pongezi, wakati wengine mkiwa mmekaa pembeni mkisikiliza sauti yangu itakayokuwa inaambatana na Piano nitakayokuwa nikiwapigia.
Lakini haya yote yatatendeka, pale tu nitakapo pata uwezo wa kifedha wa kununua Piano kubwa ya mfano wa hizo nilizo zi post au bora zaidi ya hizi.
Ningependa iwe hivyo, na nikipata nafasi ya ku SANYA, basi nita SANYA SANYA mpaka nihakikishe nimenunua Piano, Na ndipo nitakapowaalika wapendwa wangu wooooooote kuja kushuhudia hili nililoliandika leo.

Na Album itakayofuata ambayo itakuwa ni ya 6. Na ambayo mpaka sasa bado haina jina wala haijaanza kurekodiwa, baadhi ya nyimbo kutoka katika album hiyo ningependa nizipige mwenyewe kwa mikono yangu miwili. MWISHO AKASEMA

 
                                         " YOU WILL WHEN YOU BELIEVE"